Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu, Taasisi ya Umoja wa Kiislamu ya London na Chuo Kikuu cha al Azhar na unahudhuriwa na ujumbe kutoka nchi 30 duniani.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu Jafar Abdulsalam amesema kuwa mkutano huo unafanyika kwa lengo la kuonesha umuhimu wa umoja wa Kiislamu katika zama hizi na kuchunguza njia za kufikiwa umoja huo kati ya mataifa ya ulimwengu wa Kiislamu.
Abdulsalam ameongeza kuwa masuala mengine yanayojadiliwa katika mkutano huo wa kimataifa ni uchunguzi juu ya mipango ya kufikiwa umoja wa Kiislamu katika masuala ya uchumi, malezi na elimu, uchunguzi wa vizuizi vya umoja baina ya Waislamu na njia za kukabiliana na vizuizi hivyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu amesema kuwa umma wa Kiislamu unahitajia kufanyika mikutano kama hii katika kipindi cha sasa kwa ajili ya kutafuta njia za kutimiza lengo hilo.
Mkuu wa Taasisi ya Umoja wa Kiislamu ya London Kamal al Halbawi amesema kuwa tafiti na makala 40 za wasomi na wataalamu wa Kiislamu kotuka maeneo mbalimbali dunia zitachinguzwa katika mkutano huo. 1000459