IQNA

Saudi Arabia, tumaini la mwisho la Israel

23:46 - May 06, 2012
Habari ID: 2319625
Ripoti ya hivi karibuni ya Chuo Kikuu cha Tel Aviv imesema kuwa utawala wa kifalme Saudi Arabia ndio tumaini la mwisho la utawala haramu wa Israel la kulinda maslahi yake katika nchi za Kiarabu.
Ripoti hiyo imesema aghalabu ya waitifaki wa Israel katika eneo wamesambaratika na kwamba Saudi Arabia sasa ndiyo nchi pekee inayosimama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivyo ina nafasi muhimu katika kuilinda Israel.
Ripoti hiyo imesema familia ya Aal Saud ni muhimu sana kwa Israel kwani Saudi Arabia inaendeleza harakati zake katika nchi kama vile Yemen, Misri, Iraq na Lebanon kwa lengo la kupunguza ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi hizo.
Ikumbukwe kuwa mwezi Machi mwaka huu mwanazuoni wa ngazi za juu wa Misri Sheikh Mohammad Alaedin Madhi alizituhumu Saudi Arabia na Qatar kuwa zinaingilia mambo ya ndani ya nchi zingine za Kiislamu. Sheikh Madhi aliwataja watawala wa Saudi Arabia na Qatar kuwa ni watumwa wa Israel.1001056
captcha