IQNA

Kujitolea kwa Imam Hussein (as) huko Karbala kulikuwa ni kwa ajili ya kutetea haki

12:19 - May 09, 2012
Habari ID: 2322002
Imam Hussein (as), mjukuu wa Mtume Mtukufu (saw) alijitolea huko katika jangwa la Karbala kwa lengo la kutetea haki na kumridhisha Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.
Hayo yamebainishwa na Sayyid Ahmad Madhlum, gavana wa Jimbo la Jharkhand katika kongamano la 42 la kidini ambalo liliandaliwa chini ya anwani ya 'Siku ya Hussein (as)' ambapo wanazuoni, wasomi, wanafikra, watafiti na viongozi wa kidini na kisiasa walishiriki.
Kongamano hilo lililofanyika siku ya Jumatatu katika mji wa Ambid katika jimbo la Uttar Pradesh lilichunguza sira na maisha ya Imam Hussein (as).
Gavana Madhulum amesema kwamba Imam Hussein (as) alisimama na kupigana dhidi ya dhulma na kutosalimu amri mbele ya ukandamizaji na uonevu wa watawala wa zama zake. Amesema kupitia mapambano hayo dhidi ya dhulma Imam Hussein (as) aliweza kuwathibitishia walimwengu namna ya kujitolea kwa lengo la kutetea uadilifu na haki katika jamii.
Shakhsia wengine waliozungumza katika kongamano hilo ni pamoja na Wasiyu Hussan Khan Mkuu wa Chuo cha Kiarabu cha Wathiqa na Abdallah Khan, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na idadi kadhaa ya wasomi wa kidini wa nchi hiyo. 1002977
captcha