Hafla hiyo iliyofanyika Jumatatu Mei 7 iliitishwa kwa lengo la kusherehekea ushindi wa Jeshi la Sudan dhidi ya askari vamizi wa Sudan Kusini waliokuwa wameteka eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig.
Hafla hiyo iliandaliwa nna Baraza Kuu la Da'awa ya Kiislamu kwa ushirikiano na maimamu na maqari wa Sudan.
Ikumbukwe kuwa Aprili 10 vikosi vya Sudan Kusini vilishambulia na kukalia kwa mabavu mji wa Heglig. Baada ya wiki moja hivi, vikosi vya taifa la Kiislamu la Sudan viliukomboa mji huo.
Baadhi ya duru za kisiasa zinaamini kuwa hali iliyojitokeza hivi sasa kati ya Sudan na Sudan Kusini ni matokeo ya harakati ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Utawala wa Kizayuni umekuwa ukifikiria kila mara juu ya namna ya kuidhoofisha Sudan na kupata njia ya kuvifikia vyanzo vya maji ya Mto Nile. Mbali na sababu hiyo, kuwepo utajiri mkubwa wa mafuta huko Sudan Kusini pia kumezidi kuzifanya Tel Aviv na Washington ziwe na uchu na tamaa ya kujipenyeza na kujikita zaidi katika eneo.
1003921