IQNA

Ubaguzi dhidi ya Waslamu umeenea nchini Uholanzi

12:12 - May 12, 2012
Habari ID: 2323697
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika la Maurice de Hond la Uholanzi unaonyesha kwamba nusu ya wahajiri nchini humo wanabaguliwa kwa misingi ya kidini.
Kwa mujibu wa televisheni ya Press TV uchunguzi wa shirika hilo unabaini wazi kwamba Waislamu wanaoishi Uholanzi wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa kutoka kwa taasisi za serikali na jamii ya nchi hiyo tokea kuanza kuenezwa siasa na propaganda za chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, asilimia 58 ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo wanaamini kwamba muamala wa serikali na raia wa Uholanzi kuhusiana na Waislamu ni wa kibaguzi. Sehemu kubwa ya Waislamu wa Uholanzi ni wafanyakazi za mikono kutoka nchi za kaskazini mwa Afrika na Uturuki ambao wamehajiri nchini humo kwa njia zisizo za kisheria. Uholanzi kwa kawaida huwapa wahajiri uraia baada ya kuishi nchini humo kwa miaka mitano, jambo linalowawezesha kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali. 1005085
captcha