IQNA

Hujuma 200 dhidi ya misikiti Ujerumani

13:17 - May 14, 2012
Habari ID: 2325535
Misikiti ya Ujerumani ilishuhudia hujuma zaidi ya 200 kati ya mwaka 2001 hadi 2011, hujuma ambazo zilitekelezwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, kati ya hujuma hizo, 83 zimejiri katika jimbo la North Rhine-Westphalia. Aghalabu ya hujuma dhidi ya misikiti hujumuisha kupaka rangi na kuandika maandishi machafu katika kuta na kuteketeza moto misiti.
Uchunguzi uliofanywa kufuatia ombi la mrengo wa kushoto katika Bunge la Ujerumani umebaini kuwa katika kipindi hicho cha mwaka 2001 hadi 2011 kwa ujumla kulishuhudiwa hujuma mara 219 zilizotekellzwa kwa malengo ya kisiasa na watu wanaouchukia Uislamu (Islamophobes) dhidi ya misikiti na maeneo mengine ya kidini ujerumani.
Msemaji wa Sera za Ndani katika Chama cha Mrengo wa Kushoto Ujerumani amesema anaamini kuwa polisi na serikali imeonyesha kutojali kuhusuana na hujuma za watu wenye chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
1007290
captcha