IQNA

Jeshi la Kizayuni lajiandaa katika kukaribia Siku ya Nakama

17:43 - May 15, 2012
Habari ID: 2326729
Jeshi la Utawala haramu wa Israel limeajiweka tayari kukabiliana na hatari yoyote inayoweza kuzuka dhidi yake katika siku ya kuadhimishwa Siku ya Nakama ambayo ni siku ya kumbukumbu chungu ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Yaum as-Sabe' linalochapishwa Misri, msemaji wa polisi ya utawala wa Tel Aviv alisema hapo jana Jumatatu kwamba polisi hiyo inashirikiana kwa karibu na jeshi na walinzi wa mipaka ya utawala huo kwa lengo la kukabiliana na aina yoyote ya hatari inayotishia usalama wake katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu. Gazeti la utawala huo la Yediot Ahronot limesema kuwa kwa kutilia maanani mgomo wa chakula unaofanywa na mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala huo, mgomo ambao umekuwa ukiendelea kwa muda wa mwezi mmoja sasa, jeshi la utawala huo mwaka huu litashuhudia ghasia na machafuko mengi zaidi.
Leo Jumanne Mei 15 inayosadifiana na siku ya kunyakuliwa ardhi za Wapalestina na kubuniwa rasmi utawala haramu wa Israel hapo mwaka 1948, siku ambayo huitwa na Wapalestina kuwa ni Siku ya Nakba au kwa ibara nyingine siku ya maafa, maelfu ya Wapalestina huandamano kutangaza mfungamano wao na ardhi zao za jadi pamoja na azma yao ya kuendelea na mapambano hadi watakapozikomboa ardhi zao zote kutoka kwenye makucha ya walowezi wa Kizayuni. Uvamizi na uporaji wa ardhi za Waplestina hapo mwaka 1948 ulifanya watu 760,000 kati yao kuwa wakimbizi, na kufikia sasa kuna wakimbizi wa Kipalestina wapatao milioni 4.8 wanaoishi katika pembe tofauti za dunia na hasa katika nchi za Jordan, Syria Lebanon na katika ardhi zao wenyewe za Palestina. 1008452
captcha