Kwa mujibu wa gazeti la al-Wasat la Bahrain Ali al-Jabal, mkuu wa kamati ya mabaraza ya miji ya al-Wifaq amesema kwamba baraza la mji huo lilichukua hata ya kubomoa msikiti huo hapo jana asubuhi. Amesema amri ya kubomolewa msikiti huo ilitolewa na Wizara ya Mabaraza ya Miji ya Bahrain, jambo ambalo amesema ni kinyume cha sheria kwa sababu hata meya wa eneo la Shimaliya hakufahamishwa hatua hiyo. Amesema msikiti huo umebomolewa tena na askari usalama wa utawala dhalimu wa Aali Khalifa, hali ya kuwa ulikuwa unaendelea kukarabatiwa na wananchi wa Bahrain baada ya kubomolewa mara ya kwanza na askari haohao. Al-Jabal amesema msikiti huo ni wa Wizara ya Sheria ya Bahrain na kwamba umekuwa ukikarabatiwa baada ya wananchi kupata kibali kutoka kwa wakuu husika. Amesema hatua hiyo inabainisha wazi vita vinavyoendeshwa na watawala wa Aali Khalifa dhidi ya nyuma za Mwenyezi Mungu na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu. Mwanachama huyo wa al-Wifaq amesema kuwa utawala huo unaoshirikiana na wageni kukandamiza raia wa Bahrain kufikia sasa umeshabomoa misikiti 38. 1008335