IQNA

Chomsky: Bush aliteka nyara na kutesa, Obama anaua

16:44 - May 17, 2012
Habari ID: 2328023
Msomi maarufu wa Marekani Noam Chomsky amekosoa vikali hujuma ya ndege zisizo na robani (drone) za Marekani katika maeneo mbali mbali duniani na kusema utawala wa rais George W Bush ulikuwa ukiwateka nyara na kuwatesa watu nao utawala wa sasa wa rais Obama unawaua watu wasio na hatia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Noam Comsky ameliambia jarida la Democracy Now kuwa 'utawala wa Obama unapofikia uamuzi kuwa haumpendi mtu fulani, basi mtu huyo huuawa mara moja ili kuzuia kuwepo vituo vya utesaji,'.
Comsky ameukosoa utawala wa Obama kwa kumuua kinyume cha sheria Anwar al Awlaki, mwanazuoni Muislamu wa Yemen aliyezaliwa Marekani.
Ameongeza kuwa, 'Awlaki aliuawa, aliyekuwa karibu naye aliuawa. Baada ya muda mfupi mototo wake wa kiume aliuawa. Suala kuwa alikuwa raia wa Marekani halikutajwa.'
Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kushambulia Afghanistan, Yemen, Pakistan, Somalia kwa kisingizio cha kupambana na magaidi lakini wahanga wakuu wa mashambulizi hayo ni raia wa kawaida.
Mashambulizi hayo yanayofanywa na jeshi la Marekani katika nchi hizo ni kinyume cha sheria za kimataifa.
1009801
captcha