Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, muungano huo utakao julikana kama Harakati ya Kiislamu utazinduliwa rasmi Mei katika kongamano la Umoja wa Ummah na Mshikamano wa Kiislamu. Kongamano litahudhuriwa na wanazuoni wa ngazi za juu kutoka makundi ya Deobandi, Barelvi, Ahle-Hadith na Shia Ithanasheri.
Qazi Hussain Ahmad kiongozi wa zamani wa Chama cha Jamaat Islami amesema muungano huu mpya utajadili utekelezwaji mapendekezo ya Baraza la Idiolijia ya Kiislamu ambalo huishauri serikali kuhusu masuala ya sharia za Kiislamu.
Muungno huo unatazamiwa kubuni tume ya maelewano ili kusuluhisha matatizo ya kimadhehebu Pakistan.
1011957