Kwa mujibu wa gazeti la Le Mond, serikali ya Islamabad imechukua hatua hiyo kutokana na kiburi cha wasimamizi wa mtandao huo cha kuendelea kuweka kwenye mtandao huo mashindano ya vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw) licha ya kuonywa na kuombwa mara kadhaa kufuta mashindano hayo ya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu. Maafisa wa Pakistan wanasema Uislamu hauruhusu hata kidogo matukufu ya dini yoyote ile kufanyiwa dharau na kuvunjiwa heshima. 1012829