Wawakilishi wa Bahrain walioshiriki katika kikao hicho walishindwa kujibu majibu na lawama zilizotolewa dhidi ya watawala wa nchi hiyo kutokana na ukweli kwamba jinai na ukiukwaji wa haki za binadamu unaotekelezwa nchini humo dhidi ya raia wasio na hatia ni mkubwa mno kiasi kwamba hauwesi kutetewa wala kuhalalishwa kwa njia yoyote ile. Baraza hilo pia limewakosoa vikali watawala wa Bahrain kwa kutotekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kutafuta Ukweli iliyoongozwa na Mahmoud Sherif Bassiouni na pia kuongezeka kwa jela nchini humo. 1013972