Baraza hilo limechukua uamuzi huo hii leo Jumanne ambapo mufti mkuu wa nchi hiyo ambaye ni Abdul Karim Gahutu na ambaye alipewa nafasi ya kuhudumia nafasi hiyo mwaka jana sasa atahudumu katika nafasi hiyo hadi mwaka 2019. Lengo la kuongezwa muda huo limetangazwa kuwa ni kutolewa huduma zaidi kwa Waislamu wa nchi hiyo. Baraza hilo pia limebuni Baraza la Masuala ya Kijamii na Fikra ya Pamoja kwa madhumuni ya kutatua na kushughulikia masuala yanayowahusu Waislamu wa Rwanda. Lengo jingine la kubuniwa baraza hilo limetajwa kuwa ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu wa nchi hiyo. 1014214