Sherehe hiyo ambayo ilifanyika katika hoteli ya Sheraton mjini Doha aliwatunuku washindi wa mashindano hayo yaliyopewa jina la Sheikh Jassim zawadi nono. Mashindano hayo yalifanyika katika makundi tofauti ya hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tartil na tajwid, hifdhi ya juzuu 25 kwa visimo hivyo viwili, juzuu 20, 15, 10, 5 na hatimaye juzuu moja maalumu kwa watoto walio na umri wa chini miaka minane. Hatua ya mwisho ya mashindano hayo pia imefanyikaleo ambapo imewashirikisha washindani 10 ili kuainisha washindi wa mwisho. Mshindi wa kwanza amepewa riali 60,000 wapili riali 48,000 na wa tatu riali 36,000 za Qatar. Duru ya 19 ya mashindano hayo ya kitaifa na ambayo hufanyika kila mwaka ilianza tarehe 30 Aprili ambapo iliwashirikisha washindani wa kike na kiume 1500. 1013845