IQNA

Chuo kikuu Afrika Kusini chamtimua balozi wa Israel

11:45 - May 24, 2012
Habari ID: 2332991
Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal cha Afrika Kusini (UKZN) kimebatilisha hotuba iliyokuwa imepangwa ya Naibu Balozi wa Utawala haramu wa Israel nchini humo Yaakov Finkelstein.
Uamuzi huo umechukuliwa na Naibu Kansela wa UKZN Profesa Joseph Ayee kufuatia mashinikizo ya vyama vya wanafunzi na wahadhiri.
Mhadhiri mwandamizi katika Kitivo cha Sayansi za Kijamii UKZN Dkt. Lubna Nadvi amesema: 'Hii ni hatua nzuri ya UKZN. Israel inatengwa kimataifa, kama utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini ulivyotengwa, kwa hivyo hakuna anayetaka kujihusisha na Israel.'
Uamuzi wa UKZN ni pigo jingine kwa uhusiano wa Israel-Afrika Kusini ambao hivi karibuni ulizorota kutokana na uamuzi wa Afrika Kusini wa kususia bidhaa kutoka ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
1015265
captcha