Kikao hicho kitafunguliwa kwa hotuba ya Dkt. Abdulazizi Othman Altwaijri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Kielimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO. Hotuba hiyo itasomwa na Dkt. Mukhtar Ahmad Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO.
Baada ya kikao hicho cha ufunguzi Zawadi ya Mwaka 2011 ya FUIW ya Utafiti wa Chuo Kikuu itakabidhiwa Dkt. Yusuf Hayek, profesa katika Chuo Kikuu cha Al Ain cha Umoja wa Falme za Kiarabu cha na Dkt. Fatima Mahmoud Al Zayat, profesa katika Chuo Kikuu cha El-Mansoura cha Misri.
Kikao hichoo kitakadili miradi kadhaa ya utafiti hasa Chuo cha Kiislamu cha Mtandao wa Kompyuta na Bodi ya Kiislamu ya Viwango.
Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu ilianzishwa mwaka 1987 na inafungamana na ISESCO. Hivi sasa jumuiya hiyo ina wanachama 273 katika ulimwengu wa Kiislamu.
1016402