IQNA

Wanamapinduzi wa Bahrain wafunga njia kuu

18:58 - May 26, 2012
Habari ID: 2334488
Wananchi wanamapinduzi wa Bahrain jana Ijumaa walifanya maandamano na kufunga barabara kuu za katika sehemu tofauti za nchi hiyo kwa lengo la kulalamikia hatua ya ufalme wa nchi hiyo ya kuwatia mbaroni kiholela wanawake na pia uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo wa Aali Khalifa.
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Alam, jana Ijumaa sehemu nyingi za Bahrain zilikuwa viwanja vya maandamano ya kualalamikia silaha za Marekani kwa utawala huo, maandamano ambayo yalivurugwa na askari usalama wa utawala huo. Kuhusiana na suala hilo Ayatullah Sheikh Isa Qassim, Kiongozi wa Mashaia wa Bahrain amesema mgogoro wa nchi hiyo utatatuliwa tu pale watawala wa Manama watakapoamua kusalimu amri mbele ya matakwa ya wananchi. Tokea mwaka mmoja uliopita, Bahrain imekuwa ikishuhudia malalamiko na maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya ufalme kandamizi wa nchi hiyo unaoungwa mkono na majeshi ya baadhi ya nchi za Kiarabu na hasa Saudi Arabia, ambayo yanaendelea kukandamiza na kuvunja wazi haki za Wabahrain. 1016740
captcha