Azimio hilo limepitishwa kwa kura 56 za kuunga mkono, sita za kupinga, 48 zisizo za upande wowote ambapo wanachama 78 hawakuhudhuria.
Azimio hilo limeutaka utawala ghasibu wa Israel kusitisha mara moja mzingiro wake katika ardhi za Palestina hasa Ukanda wa Ghaza. WHO imesema mzingiro huo umesababisha uhaba mkubwa wa huduma za afya jambo ambalo limepelekea afya ya Wapalestina kuwa mbya huku wengi wakipoteza maisha yao. WHO imeutaka utawala haramu wa Israel kuondoa vizingiti kwa magari ya huduma za afya na wafanya kazi wa sekta ya afya huko Palestina. Aidha taasisi hiyo imeutaka utawala haramu wa Israel uboreshe hali ya wafungwa Wapalestina hasa wafungwa, wanawake, watoto na wagonjwa.
1017623