IQNA

Ukumbi mpya wa sala wafunguliwa Brazil

12:56 - May 27, 2012
Habari ID: 2335090
Ukumbi mpya wa sala umefunguliwa Jumamosi hii katika eneo la Penha mjini Sao Paulo huko Brazil.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ukumbi huo umefunguliwa katika hafla iliyomshirikisha Sheikh Al Bukai, Imamu wa Msikiti wa Pari mjini humo pamoja na Waislamu wa eneo hilo.
Sheikh Hassan Borji ,Imamu wa Msikiti wa Mohammad Rasulullah SAW katika mji wa Sao Paulo atakuwa katika ukumbi kuwa mara mbili kwa wiki kwa lengo la kusalisha sala ya Jamaa.
Ukumbi huo wa sala umefadhiliwa na Waislamu wenye asili ya Lebanon waishio nchini Brazil na moja ya malengo yake ni kuimarisha umoja wa Waislamu nchini humo na pia kuandaa mazingira ya Waislamu kujuana.
Sao Paulo ni mji mkubwa wenye idadi ya watu takribani milioni 30.
1015945
captcha