Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Canada kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Utamaduni ya Iran siku ya Jumamosi kilitayarisha kongamano la 'Qur'ani; Kitabu cha Mwamko' ambapo wasomi, wanafikra na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Canada walihudhuria.
Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Carleton mjini Ottowa.
Wazungumzaji katika kikao hicho wamesema kwamba Qur'ani Tukufu ni kitabu cha mbinguni ambacho kiliteremshwa kwa ajili ya kumjenga mwanadamu kimaanawi na kimaada duniani. Wameashiria fikra potofu na propaganda zinazoenezwa na vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya Qur'ani na kusema kuwa Wamagharibi wanaeneza fikra hizo potofu dhidi ya kitabu hiki kitakatifu cha mbinguni na kujaribu kuonyesha kuwa kinachochea vitendo vya mabavu katika hali ambayo kitabu hicho kinaeneza ujumbe wa amani, upendo, maadili mema na mwamko katika jamii ya mwanadamu. Amesema njia bora na muhimu zaidi ambayo imetumiwa na Qur'ani katika kumwamsha mwandamu ni kupambana na ujahili na ujinga, ambao humwondoa mwanadamu kwenye njia ya haki, uadilifu na maadili bora. Vikao vya maswali na majibu pia vimefanyika katika kongamano hilo. 1017583