Akizungumza na IQNA, mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati Ahmad Kazemzadeh amesema mrengo wa Machi 14 nchini Lebanon unashirikiana na Wamagharibi na Wazayuni katika kutekeleza njama dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Najib Mikati na kuibua machafuko nchini humo.
Ameendelea kusema kuwa Mrengo wa Machi 14 pia unashirikiana na Wamagharibi na Wazayuni katika kuifanya Lebanon kuwa makao ya magaidi wanaoipinga serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. Mrengo wa Machi 14 Lebanon unaongozwa na waziri mkuu wa zamani Saad Hariri.
Wakati huo huo Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, wapinzani wana nia ya kuing'oa serikali ya Lebanon madarakani. Hayo yamesemwa na Muhammad Raadi mkuu wa mrengo wenye mfungamano na Hizbullah katika bunge la nchi hiyo na kuongeza kuwa, baada ya wapinzani kushindwa kuisambaratisha harakati ya Hizbullah wameazimia kuiangusha serikali ya Najib Miqat sambamba na kuanzisha tuhuma dhidi ya jeshi na vyombo vya usalama vya nchi hiyo. Akiashiria mpango wa kuangusha serikali ya nchi hiyo Raad amesema, hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuvivunjia heshima vyombo vya usalama vya Lebanon hasa kwa kuzingatia kuwa, vikosi vya nchi hiyo vinafanya juhudi kubwa za kulinda usalama na amani wa nchi hiyo.
1017093