Mwanazuoni huyo aliuawa alipokuwa katika moja ya ofisi za Harakati ya Kiislamu jimboni humo. Mwanazuoni huyo ambaye ni ndugu yake Sheikh Mustafa Sidi alikuwa mwanachama muhimu wa jumuiya hiyo ya Kiislamu ambaye amekuwa akifanya harakati za kueneza mafundisho sahihi ya Uislamu wa Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu (saw) katika mji huo. Pia amekuwa na rekodi ya kueneza mafundisho ya watukufu hao wa Kiislamu katika miji mingine ya Nigeria. Tukio hilo linajiri katika hali ambayo wiki mbili zilizopita wanaharakati wengine wa kidini waliuawa na watu wasiojulikana na ushahidi uliopo unaonyesha kuwa mauaji hayo yanatekelezwa kwa mpangilio maalumu. Hali hiyo imezusha hofu miongoni mwa Waislamu wa mji uliotajwa na kuongeza wasiwasi kuwa huenda wanaharakai wengine wa Kiislamu wakauawa katika siku zijazo kwa njia hiyohiyo ya kigaidi. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mauaji hayo na wala sababu za kutekelezwa kwake hazijulikani. 1019964