Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa kutimia miaka 23 tangu alipofariki dunia Imam Khomein MA Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ameongeza kuwa, ana matumaini kuna siku umuhimu wa nafasi endelevu ya Imam Khomeini katika mabadiliko yote ya kieneo na hata mapinduzi ya nchi za Kiarabu, itajulikana zaidi.
Sayyid Nasrullah amemuelezea Imam Khomein kwamba alikuwa ni shakhsia adhimu, mwanafalsafa na mwanafikra mkubwa wa Kiislamu na kuongeza kwamba, Imam aliyekuwa na sifa za wazi na huku akielewa vyema umuhimu wa nchi kuwepo na uongozi na kiongozi, mara tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alichukua hatua za kujenga na kuleta maendeleo nchini Iran.
1021696