IQNA

'Wamagharibi ndio wanaohusika na operesheni za kigaidi Syria'

11:53 - June 02, 2012
Habari ID: 2339155
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema kwamba nchi za Magharibi na washirika wao ndio waliotekeleza operesheni za kigaidi za hivi karibuni nchini Syria.
Aidha sambamba na kushiaria jinai za makundi ya kigaidi nchini Syria Hujjatul-Islam Walmuslimin Kadhim Sidiqi amesema nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za kieneo zinafanya jitihada za kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuyapatia silaha makundi ya kigaidi. Sidiqi aidha amezitahadharisha nchi za eneo hili zinazoingilia masuala ya ndani ya Syria kuwa hazipaswi kuchukua hatua ambazo ni kinyume na matakwa ya wananchi wa nchi hizo. Aidha Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema kuhusiana na uchaguzi wa Rais wa Misri kuwa, kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi huo Ahmad Shafiq aliyekuwa Waziri Mkuu wa utawala uliopinduliwa wa Husni Mubarak ni suala lenye kuzusha maswali na kwamba linaonyesha uingiliaji wa nchi nyingine katika uchaguzi wa nchi hiyo.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran pia ameashiria mwamko wa 15 Khordad ambao ulikuwa cheche asili ya Mapinduzi ya Kiislamu Iran. Mwamko huo, chini ya uongozi wa Imam Khomeini MA uliannza mwaka 1963. tarehe 15 Khordad mwaka 1342 Hijria Shamsia, sawia na tarehe tatu Juni mwaka 1963, ilikuwa tarehe muhimu kiasi kwamba Imam alisema Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa ni kuendeleza mwamko wa 15 Khordad.
1021549
captcha