IQNA

Vikosi vya Bahrain vyawakandamiza waandamanaji

15:12 - June 02, 2012
Habari ID: 2339365
Vikosi vya Bahrain na Saudia vimewashambulia waandamanaji katika miji na vijiji mbali mbali vya Bahrain.
Duru zinaarifu kuwa vikosti katili vya utawala wa Aal Khalifa Ijumaa usiku vimewakandamiza wananchi waliojitokeza katika maandamano ya amani kukumbuka mwaka moja tokea sheria ya hatari ianze kutekelezwa kwa lengo la kuzima mwamko wa Kiislamu.
Matakwa ya watu wa Bahrain hayako katika fremu ya masuala ya kimadhehebu au kikabila bali watu wote wa Bahrain wakiwemo Mashia na Masunni kwa mashikamano wanataka kufikia lengo la pamoja. Wabahraini wote wanataka marekebisho ya mfumo wa utawala na kisiasa na mabadiliko ya kimsingi yatakayopelekea kuondolewa dhulma na ukosefu wa uadilifu katika jamii. Hivi sasa pamoja na mauaji , kufungwa waanndamanaji, mateso, kufutwa kazi waandamannaji na jinai zingine zote zinazotekelezwa na vikosi vya utawala wa Aal Khalifa kwa himaya ya Saudi Arabia dhidi ya taifa la Bahrain, lakini bado watu wa Bahrain wangali na moyo imara wa mapambano na wameazimia kuendeleza mapambano yao. Kuendelea mwamko wa watu wote wa Bahrain kunatokana na istikama na kusimama kidete wananchi hao wanaodhulumiwa. Kwa hakika kusimama kidete na mashikamano ni nukta muhimu katika mwamko wa watu wa Bahrain jambo ambalo limpelekea utawala wa Aal Khalifa kuchanganyikiwa. Inaelekea kuwa hatua za kimabavu kama vile kuwatia nguvuni wanamapambano, kuwafuta kazi wafanyakazi wapinzani na kuwatimua wanafunzi na hatua zinginezo zinazochukuliwa na utawala dhalimu wa Aal Khalifa, badala ya kudhoofisha wananchi zimezidisha irada imara ya waandamanaji na kuzidisha hisia za chuki dhidi ya watawala.
1022233
captcha