Katika kongamano hilo la siku mbili masuala kama vile kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kieneo katika kuboresha huduma za banki za Kiislamu ni kati ya yatakayojadiliwa.
Ravi Menon, mkurugenzi wa Halmashauri ya Masuala ya Fedha Singapore amehutubia ufunguzi wa kikao hicho. Mkuu wa Banki ya Maendeleo ya Kiislamu Ahmad Mohammad Ali Al Madani pia amehutubia kongamano hilo.
Sekta ya kifedha ya Kiislamu inastawi kwa asilimia 15 hadi 20 kwa mwaka na ni kati ya sekta za fedha zinazostawi kwa kasi zaidi duniani. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Ernst & Young kuhusu banki za Kiislamu, mtaji wa banki za Kiislamu sasa umepindukia US$ trilioni 1.1. mwaka huu hili likiwa ni ongezeko kwa asiliami 33 kutoka mwaka 2010.
1023205