Rashi Ghanouchi amesema serikali daima ikubuniwa, sheria za Kiislamu zitatekelezwa kikamilifu nchini humo.
Aidha ametoa wito wa kufanyika mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa ili kuondoa uhasama unaotawala medani ya kisiasa na kijamii nchini humo. Rashid Ghanouchi amesema kuwa malengo ya mapinduzi hayawezi kufikiwa katika anga ya mfarakano na chuki na ametaka makundi yote yanayojaribu kuwatenganisha wananchi yakome kufanya hivyo na badala yake yaketi kwenye meza ya mazungumzo kwa maslahi ya taifa.
Hii ni katika hali ambayo mwezi uliopita kundi la Masalafi lilivamia maeneo kadhaa yakiwemo makanisa, kumbi za starehe pamoja na vituo vya polisi na kuyachoma moto. Ghanouchi amesmea maridhiano ya kitaifa ndio njia pekee ya kuelekea kwenye demokrasia kamili baada ya miongo kadhaa ya dhulma na udikteta nchini Tunisia.