IQNA

Vikatuni vilivyo dhidi ya Uislamu vyakiangusha chama cha siasa nchini Ujerumani

11:58 - June 06, 2012
Habari ID: 2341018
Moja ya vyama vinavyopiga vita Uislamu nchini Ujerumani kilichotumia vikatuni vilivyo dhidi ya Uislamu kwa ajili ya kujipatia kura na kupata nafasi ya kisiasa miongoni mwa vyama vya mrengo wa kulia barani Ulaya kimeshindwa kufikia lengo lake hilo baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya On Islam, chama hicho cha Pro NRW kimeshindwa vibaya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni magharibi mwa Ujerumani. Viongozi wa chama hicho wamesema kuwa walifikia uamuzi wa kutumia vikatuni hivyo vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw) pamoja na matukufu mengine ya Kiislamu kutokana na kuwa vyama vidogo vya kisiasa nchini Ujerumani haviwezi kuvishinda vyama vikubwa kwa kutumia mbinu za kawaida. Wamesema waliamua kutumia vikatuni hivyo vinavyokejeli na kudharau matukufu ya Kiislamu kwa lengo eti la kuibua mbinu mpya ya kampeni za uchaguzi kwa lengo la kujikusanyia kura. Licha ya chama hicho kutumia mbinu na njia hizo za dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu lakini hakikupata mafanikio yoyote ya kisiasa katika uchaguzi huo. 1023544
captcha