IQNA

Rais Ahmadinejad alaani vikali sera haribifu za Marekani duniani

15:05 - June 07, 2012
Habari ID: 2341652
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani sera za kujitanua za Marekani kote duniani na kuitaja Marekani kuwa 'mbwa mwitu wa zama zetu hizi anayejaribu kuiangamiza dunia kwa pupa.'
Akihutubia wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Peking katika mji mkuu wa China, Beijing, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa 'mbwa mwitu huyu (Marekani) ameeneza vita katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa kushirikiana na Wazayuni na kulikandamiza na kulidhulumu taifa la Palestina.'
Katika kikao hicho cha Jumatani, rais wa Iran amesema, leo dunia inahitaji viongozi wanaochaguliwa na wananchi na wanaozingatia maadili mema.
Rais Ahmadinejad aliwasili China Jumanne jioni akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa lengo la kushiriki katika kikao cha 12 cha viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.
Akiweko mjini Beijing, Ahmadinejad anatazamiwa kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa China.
1024204
captcha