Mpango wa Kofi Annan mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika kadhia ya Syria ulikuwa umetathminiwa kama mpango muafaka wa kutatua mgogoro wa nchi hiyo, lakini njama chafu za nchi zinazompinga rais Assad wa Syria ni jambo ambalo limefelisha mpango huo.
Wakati huo huo Msimamo wa Russia na China kwa upande mmoja na wa nchi za Magharibi na Kiarabu kwa upande wa pili yalipelekea kikao cha Alkhamisi usiku cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria kutokuwa na matokeo yoyote. Majadiliano ya masaa 10 ya wanachama wa kudumu na wa muda wa Baraza la Usalama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Kofi Annan, mwakilishi wa pamoja wa umoja huo na jumuiya iliyotajwa kuhusu Syria yalimalizika bila kuufaidi upande wowote. Wakilishi wa Uingereza, Marekani, Ufaransa na Ujerumani katika kikao hicho walijaribu kila waliloweza ili kutekeleza nchini Syria mpango kama ule walioutekeleza Yemen dhidi ya utawala wa Abdallah Swaleh, rais wa zamani wa nchi hiyo. Katika kikao hicho, Nabil al-Arabi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu alizungumzia kwa mara ya kwanza, suala la kuondolewa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Asad wa Syria. Bani Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa badala ya kuchukua msimamo usiopendelea upande wowote katika kikao hicho, alijiunga moja kwa moja na nchi za Magharibi kwa kutaka mpango wao wa kumwonda madarakani serikali halali ya Damascus utekelezwe haraka iwezekanavyo. Jambo lililowapelekea Wamagharibi washinikize hata zaidi suala la kuondolewa madarakani Rais Bashar Asad ni matamshi ya hivi karibuni ya Kofi Annan aliyesema kuwa mpango wake wa amani wa vipengee sita haujatekelezwa. Annan aliituhumu serikali ya Syria kuwa ndiyo inayochochea ghasia na kuzuia kurejea amani nchini humo. Kuvurugwa njia za kisiasa za kutatuliwa mgogoro wa Syria ni hatua ya kwanza ya nchi za Magharibi kuingilia kijeshi nchi hiyo, jambo linalochukuliwa na Russia na China kuwa hatari kubwa kwa maslahi yao katika Mashariki ya Kati. Ni kutokana na ukweli huo ndipo nchi mbili hizo wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama zikatumia kila njia ili kufanikisha mpango wa amani wa Kofi Annan nchini Syria. Kutokana na kuwa Annan amekataa tamaa kuhusiana na mpango wake mwenyewe, Warussia wamependekeza mpango mwingine wa amani kwa ajili ya kutatua mgogoro huo wa Syria. Akizungumzia suala hilo, Vitaly Ivanovich Churkin Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema Moscow hivi karibuni itakuwa mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria. Russia inatambua vyema kwamba wanachama wa kudumu wa Magharibi katika Baraza la Usalama ndio wanaozuia kupatikana ufumbuzi wa kidiplomasia wa mgogoro wa nchi hiyo ya Kiarabu. Ni kwa kutilia maanani ukweli huo ndipo viongozi wa Russia wakatafuta njia nyingine zilizo nje ya baraza hilo ili kupata uungaji mkono wa kimataifa kwa ajili ya kutatua kwa amani mzozo wa Syria. Russia na China zinapinga vikali kutumiwa njia za kijeshi katika kutatua mgogoro wa ndani wa Syria na kusisitiza kuwa zitaendelea kutafuta njia za kisiasa ili kutatuliwa kwa amani mgogoro huo unaochochewa na nchi za Magharibi na vibaraka wao wa Kiarabu.
1023387