IQNA

Ubaguzi wa rangi wa serikali ya Ubelgiji dhidi ya Waislamu

18:05 - June 09, 2012
Habari ID: 2342930
Baada ya kupiga marufuku vazi la Kiislamu la hijabu katika shule na idara za umma pamoja na kupigwa na kutusiwa wanawake wa Kiislamu wanaovalia hijabu kwenye vituo vya usafiri wa umma, serikali ya Ubelgiji inaendelea kutekeleza sheria zinazowakandamiza Waislamu nchini humo.
Kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanamke mmoja wa Kiislamu alipigwa na kukosewa heshima katika kituo kimoja cha basi nchini humo Waislamu wamekusanyika na kufika kwenye kituo cha polisi kilicho karibuna kituo hicho cha basi wakitaka mwanamke huyo wa Kiislamu aachiliwe huru mara moja. Kufuatia malalamiko ya Waislamu kuhusu suala hilo, askari usalama wameingilia kati na hivyo kuzusha mvutano na ghasia kati ya pande mbili. Baada ya kuona kwamba Waislamu wanadhulumiwa na kutiwa nguvuni bila sababu muhimu, taasisi za Kiislamu zimelalamikia vikali suala hilo jambo ambalo limepelekea polisi kuwatia nguvuni baadhi ya viongozi wa taasisi hizo kwa tuhuma za kuwa na misimamo mikali. Suala hilo limethibitisha wazi kwamba madai na nara za serikali ya Ubelgiji za kufanya mazungumzo na kuleta maelewano kati ya wafuasi wa dini tofauti za nchi hiyo ni madai na nara tupu zisizo na msingi wowote. 1025404
captcha