Terry Jones, kasisi mwenye chuki kali dhidi ya Uislamu na naysiamia kanisa moja dogo katika Jimbo la Florida nchini Marekani amesema Rais Obama anastahili kunyongwa kutokana na misimamo yake anayodai kwamba inakwenda kinyume na mafundisho ya Kikristo.
Amesema Rais huyo anapasa kunyongwa kwa kuwa eti ni adui wa Marekani, ametoa amri ya kuuawa watoto wachanga akiwa na maana na kuavya mamba, na kwamba anaunga mkono pia Uislamu ulio na misimmao ya kupindukia mipaka. Kasisi huyo ambaye amechoma moto Qur'ani Tukufu mara adhaa ameendelea kudai kwamba Obama anaiangamiza Marekani na kwamba kwa sababu hiyo inatosha kumfanya aondolewe madarakani ili kuinusuru Marekani. Ametaka apewe kura za Wamarekani katika uchaguzi ujao ili atekeleze lengo hilo. Terry Jones ametoa matamshi hayo katika hali ambayo sheria za Marekani zinachukulia tishio dhidi ya rais wa nchi hiyo kuwa ni hatia, kosa ambalo lina adhabu ya kifungo cha jela cha kati ya miaka mitano hadi kumi. Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa matamshi ya kasisi huyo yamevuka mipaka ya uhuru wa kusema. Hii ni katika hali ambayo kasisi huyohuyo ambaye ametoa matamshi ya kashfa dhidi ya Qur'ani Tukufu na hata kukichoma moto kitabu hicho cha mbinguni hajachuliwa hatua yoyote ya kisheria hadi sasa, na wala vyombo hivyo vya habari havijaitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji mipaka ya uhuru wa kusema. 1025521