Kwa mujibu wa Redio Huru ya Iraq, waandamanaji wakiwemo wawakilishi wa jumuiya na mashirika muhimu ya kiraia ya Iraq, walilaani vikali uingiliaji wa Saudia katika masuala ya ndani ya nchi hiyo na hasa yanayohusiana na siasa. Wameutuhumu utawala wa Aal Soud kwamba unafanya njama ya kuvuruga hali ya kisiasa ya Iraq na kuzusha fitina na mifarakano kati ya mirengo tofauti ya kisiasa ya nchi hiyo. Wameitka serikali kuchukua hatua za lazima kwa lengo la kuzuia uingiliaji huo wa moja kwa moja wa serikali ya Saudia katika masuala ya ndani ya nchi hiyo. Wamesema Wairaqi wenyewe wana uwezo wa kujiendeshea nchi hiyo na kwa hivyo hawahitaji uingiliaji wa nchi jirani katika uendeshaji wa mambo yao. 1026527