IQNA

Wamagharibi waendelea kusilimu

18:22 - June 10, 2012
Habari ID: 2343726
Takwimu zinaonyesha kwamba licha ya mibano na chuki zinazoenezwa na nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu lakini idadi kubwa ya watu wa nchi hizo wamekuwa wakivutiwa na kuingia kwa wingi katika Uislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya On Islam mwaka 2009 pekee watu 40,000 walisilimu nchini Uingereza,, 70,000 Ufaransa na watu laki moja huko Marekani. Ripoti hiyo inasema Hamima Goldsmith, binti milionea wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja wa watu waliosilimu. Binti huyo anasema kwamba wanawake wengi wa nchi za Magharibi hutafuta raha na ladha ya maisha katika masuala ya kimaada na kudai kwamba kutokuwepo kwa hali kama hiyo katika nchi za Kiislamu ni ukiukaji wa wazi wa haki za wanawake, jambo ambalo amesema ni kinyume kabisa na thamani za kibinadamu. Amesema Uislamu unampa mwanamke thamani kubwa na kumpa haki sawa na za mwanamke kwa misingi ya uadilifu. 1015322
captcha