IQNA

Semina ya 'Imam Khomeini na Mwamko wa Kiislamu' yafanyika Kenya

17:08 - June 12, 2012
Habari ID: 2345314
Semina yenye anwani ya 'Mtazamo wa Imam Khomeini MA Kuhusu Mwamko wa Kiislamu na Mustakabali Wake' imefanyika nchini Kenya.
Kwa mujibu wa tawi la IQNA katika Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), semina hiyo imeandaliwa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 23 wa kuaga dunia Imam Khomeini MA.
Kati ya waliohudhuria semina hiyo ni Hassan Omar, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Bw. Khamusi Mkuu wa Shirika la Uenezaji Uislamu, Bw. Givzad Balozi wa Iran nchini Kenya, Bw. Omidi Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya na Bw. Asghari ambaye ni Naibu Mkuu wa ICRO.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Waislamu wa Kenya katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, wazungumzaji waliashiria nukta kadhaa kuhusu namna Imam Khomeini MA alivyoathiri mwamko wa Kiislamu. Aidha pambizoni mwa semina hiyo kumefanyika mashindano ya kusoma kitabu.
1026850

captcha