Mufti huyo Muhhamad al-Ureifi amesema kwamba kila mhubiri wa Kiwahabi amepewa riali 1000 hadi 1500 za Saudia kwa lengo la kupambana na fikra za Kishia na kuenea kwake katika maeneo ya makazi ya Wahuthi katika vijiji hivyo.
Wayemen wamekasirishwa mno na matamshi hayo ya al-Ureifi ambayo wameyataja kuwa uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya Yemen na kuongeza kuwa anataka kuchochea fitina za kimadhehebu nchini humo.
Wahuthi wa Yemen wamekuwa wakiituhumu mara kwa mara Saudia kwamba inaingilia masuala ya ndani ya Yemen kupitia wahubiri wa Kiwahabi na wanajeshi wa nchi hiyo.
Huko nyuma Saudia iliwaruhusu askari wa Yemen kutumia ardhi yake kwa ajili ya kuwakandamiza kijeshi Wahuthi. Magenge ya Masalafi ambayo yanapewa silaha na serikali ya Riyadh pia yamewashambulia Wahuthi mara kadhaa. 1033868