IQNA

Magaidi wamuua mwanazuoni wa Kishia mjini Damascus

17:20 - June 20, 2012
Habari ID: 2350825
Magaidi wamemuua mwanazuoni mmoja wa Kishia karibu na Haram ya Bibi Zainab huko Damascus mji mkuu wa Syria.
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Alam, magaidi hao walishambulia na kumuua Abdul Quddur Jabbara pamoja na ndugu yake karibu na haram takatifu ya Bibi Zeinab (as).
Hivi karibuni pia magaidi walilipua gari moja lililokuwa limetegwa bomu karibu na haram hiyo na kuwajeruhi watu wanne.
Wakati huohuo jeshi la Syria linaendeleza operesheni za kufagia magaidi katika mitaa tofauti ya mji wa Homs. Kuhusiana na suala hilo maafisa wa Syria wametangaza kuwa jeshi limefanikiwa kuusafisha mtaa wa Sultaniya kutokana na magenge hayo ya kigaidi. 1034026
captcha