IQNA

Dikteta Mubarak akaribia mauti

17:24 - June 20, 2012
Habari ID: 2350906
Taarifa kutoka mjini Cairo Misri zinaarifu kuwa mapigo ya moyo ya dikteta Hosni Mubarak aliyepinduliwa madarakani nchini Misri yalisimama jana usiku wakati alipowasili katika hospitali ya jeshi huko kusini mwa Cairo.
Mubarak jana usiku alihamishiwa katika hospitali ya Maadi baada ya kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumulia huko katika hospitali ya jela ya Torah mjini Cairo.
Afisa mmoja wa jela amenukuliwa akisema kuwa madaktari wamemuwekea Mubarak mashine ya kupumulia ili kusaidia kuhuisha mapigo yake ya moyo.
Dikteta Hosni Mubarak aliye na umri wa miaka 84 amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupumua, shinikizo la damu, msongo wa mawazo na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida tangu ahukumiwe kifungo cha maisha jela tarehe Pili mwezi huu kwa kosa la kuua raia karibu 900 waliokuwa wakiandamana katika mapinduzi ya nchi hiyo ya mwaka uliopita.
1033910
captcha