Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la Le Figaro, Hizbullah imetoa pongezi zake za dhati kwa Mursi na kuelezea matumaini yake kwamba kwa ushindi wake huo nchi hiyo itarejea katika nafasi yake halisi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Hizbullah imewapongeza wananchi wa Misri kwa kumchagua Mursi kuwaongoza na kuelelezea matumaini yake kwamba hatua yao hiyo itachangia pakubwa katika kuirejesha Misri ambayo ni nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu kati ya nchi za Kiarabu, katika nafasi yake halisi katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.
Hizbullah ambayo haikuwa na uhusiano mzuri na utawala wa dikteta Hosni Mubarak imeendelea kusema kwamba, kung'olewa madarakani kwa dikteta huyo kuliwafurahisha mno wanachama wa harakati hiyo ya Kiislamu kwa sababu ilikuwa ikitiwa wasiwasi mkubwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hiyo na utawala ghasibu wa Israel kutokana na mkataba wa Camp David. Imesema ushindi wa Mursi unaweza kuimarishaa uhusiano wa harakati hiyo na Kiislamu na Misri. 1038251