IQNA

Zanzibar yaanzisha mfuko wa Zaka

17:34 - July 03, 2012
Habari ID: 2359788
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa serikali yake imeanzisha mfuko maalumu wa zaka ili kutekeleza wajibu wetu kwa Mola na kuzingatia manufaa mengine kwa jamii.
Kwa mujibu wa toleo la hivi karibuni la gazeti mashuhuri la Waislamu Tanzania la An-Nuur, Rais Shein amesema kuanzishwa mfuko huo ni hatua muhimu katika historia ya Zanzibar.
Akihutubu wakati wa kuzinduliwa mfuko huo katika mji wa Zanzibar, Shein ameongeza kuwa Zaka ina umuhimu mkubwa katika Uislamu. Amesema ni jambo la kusikitisha kuwa Zaka haijapewa uzito unaostahiki katika jamii.
Shein ameongeza kuwa serikali yake inataka kutumia fursa ya utoaji wa zaka ili kupunguza umasikini Zanzibar. Ameendelea kusema kuwa utoaji zaka katika jamii una mchango mkubwa katika kuinua maisha ya watu. Shein ametoa wito kwa wanaojiweza Zanzibar kuchangia Mfuko wa Zaka. Ameendelea kwa kuishukuru Ofisi ya Wakfu Zanzibar kwa jitihada zake za kufanikisha uanzishwaji Mfuko wa Zaka.
Rais Shein aliongeza kuwa: ‘Inaridhisha kusikia kuwa tayari kuna kiasi cha fedha ambazo zimeshachangwa na watu mbalimbali kwa ajili ya mfuko huu na mipango imeshatayarishwa juu ya namna bora ya kuzihifadhi amana hizi, kuzitumia kwa utaratibu na maelekezo
maalum na pia kuwepo kwa utaratibu wa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Zaka Zanzibar unakuwa endelevu’.
1043222
captcha