Katika taarifa hiyo Hizbullah imesema kuwa magaidi wamelenga mustakbali wa taifa la Iraq kupitia vitendo vya kigaidi. Hizbullah imewataka Wairaqi wawe na subira na wasiwape magaidi na waungaji mkono wao wa nje mwanya wa kueneza fitina na kuvuruga usalama wa nchi hiyo.
Imesikitishwa na ukweli kuwa licha ya magaidi kuendelea kumwaga damu ya Wairaqi lakini jamii ya kimataifa imeamua kukaa kimya bila kusema lolote kuhusiana na ugaidi huo. Hizbullah imesema kuwa ugaidi huo unaotekelezwa dhidi ya taifa la Iraq unatekelezwa kwa ushirikiano kamili wa askari vamizi wa Marekani wanaoendelea kudhibiti hali ya mambo nchini humo.
Tunakumbusha hapa kwamba mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye lori katika soko la mboga na matunda mjini Diwania ulipelekea kuuawa watu wapatao 30 na kujeruhi wengine wengi wakiwemo wanawake na watoto.
Milipuko mingine miwili uliyotokea kwenye soko la mboga na matunda mashariki mwa mji mtakatifu wa Karbala imepelekea kuuawa watu 16 na kujeruhiwa wengine 40. 1044712