IQNA

Austria yaadhimisha miaka 100 ya Sheria za Kiislamu

6:19 - July 05, 2012
Habari ID: 2361016
Serikali ya Austria imesherehekea pamoja na Waislamu wa nchi hiyo miaka 100 ya kupitishwa sheria ya kutambuliwa rasmi sheria za Kiislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.
“Austria ni mfano wa kuigwa Ulaya katika kuamiliana na Uislamu, aidha Waislamu wa Austria ni kigezo Ulaya", amesema Omar al Rawi diwani katika mji wa Vienna.
Matamshi ya Al Rawi yamekuja baada ya serikali ya Austria kuandaa sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya kutambua Uislamu kama dini rasmi nchini humo.
Kwa mujibu wa sheria za Austria, Waislamu wana haki sawa na wafuasi wa dini zingine zilizotambuliwa rasmi nchini humo kama vile Wakatoliki, Walutheri, Mayahudi na Mabudha.
Jamii ya Waislamu Austria imetajwa kuwa ya kipekee kwani sheria za nchi hiyo zinawapa Waislamu haki nyingi ikiwa ni pamoja haki ya kusoma katika shule za serikali, kujisimamia katika masuala yanayohusu Waislamu na kutengewa sehemu maalumu za ibada.
Sheria hiyo ilianza kutumika mwaka 1912 chini ya Mfalme wa Habsburg Franz Joseph baada ya Austria kuchukua udhibiti wa nchi ya Waislamu ya Bosni-Herzegovina. Kwa mujibu wa sheria hiyo Waislamu wote wanaofuata madhehebu ya Suni na Shia wanatambuliwa rasmi na wana haki kamili kama raia wengine wa Austria.
1044353
captcha