Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa Tehran na kubainisha kwamba, kuzima fitina, kusambaratisha njama na kukwamisha mipango ya kijasusi ya maadui dhidi ya mfumo na taifa la Iran ni miongoni mwa majukumu makuu ya vikosi vya usalama vya Iran.
Ayatullah Kashani ameashiria pia vikwazo vya upande mmoja vya Wamagharibi dhidi ya Iran na kusema, madola ya Magharibi yanapaswa kufikiri kimantiki kwani kinyume na hivyo yanawadhuru wananchi wa nchi zinazotekeleza vikwazo na wananchi wa nchi nyingine.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amewataka Wamagharibi watambue haki ya Iran ya kustafidi na teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani; kwani Tehran haitafumbia macho hata kidogo haki zake.
1046074