Ahmad Tubassi wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya Tadamun amesema miezi ya Machi na Juni ilishuhudia ongezeko kubwa la ukatili wa vikosi vya Israel ambavyo kawaida huwalenga raia wa Palestina wasio na hatia.
Taasisi ya Tadamun imelaani vikali sera za kibaguzi za utawala haramu wa Israel na kusema jinai za Israel dhidi ya watu wa Palestina ni ukiukwaji wa wazi wa mikataba ya kimataifa kuhusu kuwalinda raia wakati wa vita.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza jinai zake dhidi ya Wapalestina kwa kutumia hali iliyopo hivi sasa katika nchi za Kiislamu na kutokana na kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai za utawala huo.
Ni jambo linalojulikana wazi kwamba utawala wa Kizayuni hauheshimu kabisa masuala kama amani, mazungumzo, utulivu na usimamishaji vita, bali mara zote umekuwa ukitumia vitu hivyo kama njia tu ya kununua wakati wa kuuwezesha utawala huo kufanya ukatili mkubwa zaidi dhidi ya Wapalestina.
Jambo jengine linalowafanya Wazayuni wafanye jinai zao bila ya kujali chochote, ni kimya cha jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa. Ingawa jinai hizo za Wazayuni zinawaletea matatizo mbalimbali Wapalestina, lakini kamwe haziwezi kuutia doa msimamo makini wa taifa la Palestina wa kusimama imara katika kupigania malengo yake matukufu ya kukomboa kila shibri ya ardhi yake inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
1045946