Ali Akbar Velayati Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Kimataifa amesema pambizoni mwa Kikao cha Baraza la Ushauri la Mwamko wa Kiislamu kuwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu wamealikwa na sekretarieti ya baraza hilo na kwamba wakiwa hapa nchini washiriki wa mkutano huo watapata fursa ya kuitembelea miji ya Mash-had, Isfahan na Tehran.
Velayati amesema kuwa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu utachukua maamuzi makubwa kwa ajili ya wanawake na kuongeza kuwa ufuatiliaji wa ufumbuzi wa matatizo na masuala yanayowahusu wanawake ni moja kati ya malengo yenye umuhimu mkubwa ya kikao hicho. Kwa mujibu wa ripoti hiyo Kikao cha Baraza la Ushauri la Mwamko wa Kiislamu kimeanza shughuli zake leo alasiri hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na wanaharakati kutoka nchi 80 duniani.
1049302