IQNA

Hizbullah yakanusha madai mapya ya Marekani

16:55 - July 11, 2012
Habari ID: 2366413
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetupilia mbali madai mapya yalitolewa hivi karibuni na Marekani dhidi yake na kusisitiza kuwa madai hayo hayana maana wala msingi.
Kwa mujibu wa gazeti la ad-Dastur linalochapishwa Misri, Hizbullah imetoa taarifa ikisema kuwa madai hayo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani ni uongo mtupu usio na ukweli wowote.
Harakati hiyo vilevile imesisitiza katika taarifa yake kwamba uongo wa hivi karibuni uliotolewa na wizara iliyotajwa dhidi ya Hizbullah una lengo la kuiharibia jina harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu machoni pa walimwenguni.
Wizara ya Fedha ya Marekani imeituhumu Hizbullah kwamba inahusika na vitendo vya usafishaji pesa na ulanguzi wa madawa ya kulevya nchini Lebanon na Mashariki ya Kati! 1050364
captcha