IQNA

Kikao cha Benki za Kiislamu Afrika kufanyika Djibouti

16:23 - July 15, 2012
Habari ID: 2368770
Fursa na changamoto katika mfumo wa benki za Kiislamu na mfumo wa kifedha wa Kiislamu barani Afrika ni masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kikao kilichopangwa kufanyika nchini Djibouti.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho kilichoandaliwa na Benki Kuu ya Djibouti kina anwani ya ‘Mkutano wa Kilele wa Benki za Kiislamu Afrika’. Mkutano huo umepangwa kufanyika Novemba 6 na 7 mwaka huu a 2012.
‘Kwa muongo mmoja sasa biashara kati ya nchi za Afrika na nchi zingine za dunia imeimarika sana na hii inajumuisha asilimia 170 ya ongezeko la biashara na nchi za Ghuba ya Uajemi,’ amesema mkurugenzi mtendaji wa kongamano hilo David McLean.
Ameongeza kuwa hivi sasa nchi za Afrika zinabadilika kutoka kuwa tegemezi hadi kuimarisha biashara na uwekezaji na chi za Mashariki ya Kati na kwa hivyo mfumo wa kifedha wa Kiislamu unaweza kuwa na nafasi muhimu katika biashara baina ya pande hizi mbili.
1052302
captcha