IQNA

Changamoto ya wanariadha Waislamu katika Olimpiki

11:24 - July 20, 2012
Habari ID: 2372574
Wakati michezo ya Msimu wa Joto ya Olimpiki itakapoanza baadaye mwezi huu mjini London, Waislamu kote duniani, wakiwemo wanariadha bingwa, watakuwa wanatekeleza ibada ya Saumu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wanariadha Waislamu katika Olimpiki watashiriki katika mashindano ya hali ya juu huku wakiwa wanajizuia kula na kunywa mchana katika michana mirefu ya msimu wa joto London.
Kutokana na kuamka mapema kula daku, takriabni saa kumi usiku kwa saa za London, Wanariadha wengi pia wanatazamiwa kukumbwa na tatizo la kukosa usingizi.
Mohammad Abdul Bari Mkuu wa msikiti mkubwa zaidi London ambaye pia ni mwanachama wa Kamati Andalizi ya Olimpiko London amesema wanariadha Waislamu wanapaswa kuuliza wanazuoni na wataalamu wa fiqhi kuhusu suala la saumu katika mazingira watakayokumbana nayo.
Walioandaa michezo ya Olimpiki London wamesema kuna mipango wa kuwasaidia wanariadha Waislamu wanaofunga. Mbali na kuwepo migahawa ya chakula halali masaa 24, vile vile kutakuwa na vyakula maalumu vya kufuturu katika viwanja vyote vya michezo.
Mbali na wanariadha Waislamu wengine wanaofunga katika michezo ya Olimpiki London ni watazamaji, wafanyakazi, madaktari, makocha, wapishi n.k
1056655
captcha