IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ataka OIC ichukue hatua kuhusu Myanmar

14:44 - July 21, 2012
Habari ID: 2373770
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ametaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ichukue hatua imara kuwatetea Waislamu wanaouawa kinyama na kudhulumiwa nchini Myanmar.
Akuhutubu katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran Ayatullah Ahmad Khatami pia ameitaka serikali ya Myanmar iheshimu haki za Waislamu walio wachache. Maelfu ya Waislamu wameuawa nchini Myanmar na malaki ya wengine kukimbia makazi yao katika hujuma inayofanywa na Mabudha dhidi ya jamii ya Waislamu.
Kwingineko katika hotuba yake Ayatullah Khatami amelaani mashambulizi ya kigaidi ya siku ya Jumatano iliyopita nchini Syria ambapo mawaziri wawili muhimu waliuawa.
Ayatullah Khatami amesema Syria inahujumiwa kutokana na misimamo yake ya kuwatetea wanyonge na wanaodhulumiwa kama vile Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na wananchi wa Palestina.
Ameongeza kuwa mashambulizi ya kigaidi ya wiki hii huko Damascus yanaonesha jinsi nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu zinavyohitari kumwaga damu ya watu wa Syria badala ya kutatua mgogoro ulioko kwa njia ya mazungumzo.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono serikali na watu wa Syria katika juhudi zao za kutetea uhuru wa kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na wageni.
Ayatullah Ahmad Khatami aidha amepongeza hatua ya Russia na China ya kupinga azimio la kuiwekea vikwazo Syria.
1057752
captcha