IQNA

Qur'ani ya karne ya 16 yagunduliwa Uturuki

17:24 - July 23, 2012
Habari ID: 2375755
Nuskha moja ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani imegunduliwa katika uchimbaji wa ngome moja ya kihistoria huko katika mji wa Kemah katika mkoa wa Arzanjan nchini Uturuki.
Ugunduwaji wa kitabu hicho kitakatifu pamoja na maandishi mengine ya kihistoria ulifanywa siku ya Jumamosi na timu moja ya wataalamu wa mambo ya kale wa Chuo Kikuu cha Ataturk.
Qur'ani hiyo iliyogunduliwa ikiwa imefungwa kwenye kitambaa maalumu imepelekwa katika kitengo cha utafiti wa maandishi ya kihistoria yaliyoandikwa kwa mkono katika chuo kilichotajwa. Akizungumzia suala hilo, Dakta Huseyin Yurttas, mhadhiri wa masuala ya kihistoria katika Chuo Kikuu cha Ataturk na mkuu aliyesimamia timu ya uchimbaji katika ngome hiyo ya kale, amesema vitu vingine vilivyopatikana katika uchimbaji huo ni pamoja na nakala kadhaa za Qur'ani zlizoandikwa kwa maandishi ya dhahabu za karne za 18 na 19 na vilevile vitabu kadhaa vya fiqhi, itikadi na maudhui nyingine za Kiislamu. 1060165
captcha